breking news

Shirika la riadha la kenya

Shirika la Riadha la Kenya
linalojulikana kama AK ni jumuia
linazosimamia Riadha nchini Kenya.
Shirika hili ni memba wa IAAF na
Shirikisho la Riadha Afrika. AK
huratibu mashindano ya Riadha
nchini Kenya. Pia hutuma timu ya
Kenya kushiriki katika mashindano ya
kimataifa. Isaiah Kiplagat ndiye
mwenyekiti sasa hivi wa Riahda
nchini Kenya. AK ina ofisi zake kuu
katika Riadha House, karibu na
Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo, Nairobi .
Historia
Shirika hili lilikuwa likijulikana kama
Shirikisho la Amecha Kenya mpaka
mwaka wa 2002. Shirikisho
ilianzishwa katika ukoloni Kenya
mwaka wa 1952 na marehemu Derek
Erskine.
Kenya ni taifa lenye ustadi katika
Riadha, lakini talanta hii huishia
katika mbio za mbali. Wanariadha
maarufu wa Kenya kwa kawaida
hutoka wilaya kama Keiyo, Marakwet
na Nandi katika magharibi ya Kenya.
Karibu wote huwa kabila la Kalenjin.
Mashindano makuu ya kwanza ya
kimataifa ambako Kenya ilishiriki
ilikuwa michezo ya Ulaya ya 1954,
huko Cardiff, lakini Kenya
haikushinda medali yoyote.
Mashindano ya Kenya hufanyika
katika misimu ya joto, lakini majaribio
tofauti hutumika kubaini wanariadha
kwa michuano ya kimataifa.
Wanariadha mabingwa wa Kenya kwa
kawaida huhudhuria matukio hayo,
manake wale wanaozikosa huenda
kuwa wanakosa michuano mikubwa
vilevile. Wanariadha wengi wa Kenya
hushindana Ulaya, michuano ya
kitaifa na majaribu ni tukio tu
ambapo watazamaji wanaweza
kuwatazama wakishindana.
Mashindano mengine yanayoandaliwa
na Shirika la Riadha la Kenya ni kama
mfululizo wa mbio za nyika na
zingine za barabarani. Kenya
husimamia matukio ya mbio mara
tatu kila mwaka. Mbio za nyika za
Nairobi ilianza majuzi, lakini sasa
inaongoza katika ushindani na
ushiriki. Zingine ni Mbio za nyika za
Mombasa na ile ya Ziwa Kuu,
inayofanyika mjini Kisumu. Isitoshe,
kuna ushindani unaojulikana kama ,
ambayo inahusisha mashindano
mawili sawa na (42 km) na nusu
Mbio za nyika, lakini ni mbio ya nyika
kwa hivyo haiwezi linganishwa na
Mbio za nyika. Hata hivyo, tukio la
Mbio za nyika za Lewa limewavutia
wakenya wakimbiani wengi wa
kimataifa na limeshindwa na Paul
Tergat, Catherine Ndereba na Joyce
Chepchumba katika miaka iliyopita.
Wakimbiaji wengi wakenya
hujihusisha na mashirika ya kiserikali
kama vile Jeshi la Kenya, shirika la
magereza Kenya au Polisi wa Kenya,
ambayo huwapa riziki pamoja na
mazoezi. Aidha, kuna vilabu binafsi
kadhaa vya riadha, kama vile Mfae
(mjini Nyahururu) na Kiptenden
(inayopatikana Kericho).

No comments